Thursday, October 4, 2012

Maendeleo nchini Kenya




Kenya ni nchi tukufu na yenye baraka sana. Tulipopata uhuru kutoka kwa Wabeberu ilikuwa ni hatua kubwa sana bila shaka. Lakini labda hiyo hatua iliishia hapo maana uongozi katika Jamuhuri ya Kenya umekuwa ukikubwa na mizozo tangu siku za hayati Mzee jommo Kenyatta. Kenyatta na waliomzingira ama kweli waliujenga msingi wa Kenya kwa kila hali. Msingi wa maendeleo sambaba na ule wa chuki chanzo chake ni katika wakati huu. Ni dhahiri kuwa mwanzo wetu kutoka enzi za kupata Uhuru haukuenda vyema.

Kenyatta alipofariki Agosti 22 1978 aliyekuwa Makamu wake Daniel Arap Moi alichukua usukani. Bwana Moi ama kweli "alifuata nyayo" za Kenyatta. Kufuata Nyayo hizo ndicho kiini cha uhasama na kukosa maendeleo nchini mwetu. Moi aliipinga demokrasia lakini mageuzi yalipatikana mwanzoni wa 1990. Uchaguzi wa kwanza katika nchi ya Kenya mnamo Dicemba 1992 ilikuwa ni hatua kubwa. Demokracia ni hali mzuri ya kuleta mabadiliko lakini mabadiliko huanzia kwenye fikira. Hamna dhihirisho kamili ila kuangalia waliopigania mageuzi kabadilika na kuwa walaghai pia. Ulaghai wa viongozi hawa waonyesha kuwa mabadiliko ilikuwa tuu jina ila hamna aliyeamini sera hizo.

Rais Moi alipotoka kwenye uongozi, wakenya wote walishikana na kumpigia kura Rais Kibaki. Wakenya walipatia Kibaki kazi ya kuiendelesha Kenya kwa moyo wote. Uongozi wa Kibaki ulikubwa na shinda wakati Rais alipochaguwa kutotimiza mjandala waliokuwa wamekubaliana na kiongozi wa LDP bwana Raila Amolo Odinga. Inasemekana kuwa waliozingira rais Kibaki ndio waliochangia kwenye hili jambo. Shinda kubwa ya Kenya basi ilianzia hapa. Baada ya miaka tano katika uongozi wa Kibaki uchaguzi wa mwaka wa 2007 ulipindua ukurasa mpya nchini Kenya. Ukurasa huu umejaa chuki, ukabila na siasa za mgawanyiko. Vita za Kikabila zilizotokea baada ya uchaguzi zaonyesha kuwa siasa zetu bado hazijakomaa na demokracia imebaki kuwa jina ambalo halijapatikana kwenye kamusi ya Uongozi wetu.

Kenya inaelekea kufanya uchaguzi katika mwaka ujao mnamo 04/Machi/2012. Kwa kuongalia ulingo waki-siasa nchini, ni dhahiri kuwa Wakenya bado hawako tayari kwa uongozi. Wakenya wanaelekea kuchaguwa viongozi wa Kikabila ila sio viongozi wa nchi. Kila kabila laonekana kupigia ndembe anayeungwa na viongozi wa kabila lao. Katika Karne hii, hiyo sio Demokracia.

Wakenya wote watakaochaguana yafaa wachague Kiongozi ambaye ana sera mzuri za uongozi, Sera ambazo zitaleta mabadiliko ambayo Wakenya waliopigania Uhuru wangetaka kuona. Huu sio wakati wa chuki, Huu sio wakati wa makabila kujigamba, Huu sio wakati wa "watu wetu" ila huu ni wakati wa kupatia Kenya kiongozi anayefaa.

Vijana wanajukumu kubwa sana katika hili taifa. Kwanza Kenya isipoendelea ni vijana watateseka sana maanake ndio watakao rithi nchi ambayo kafirisika. Lazima vijana walete agenda mpya, yafaa vijana wachague maendeleo maanake nadhani hilo ndilo jambo la maana.

 Baada ya kuchaguwana wananchi watakaa miaka mitano ingine na malalamiko? Kura na masomo ndiyo silaha ya kweli. Mungu aibariki Kenya yetu Milele.